RAIS MWINYI AFANYA MAZUNGUMZO NA MADAKTARI WA UPASUAJI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa bado kuna kazi kubwa inayohitaji kufanywa ili kuwa na wataalamu wa kutosha hasa katika utoaji wa huduma za upasuaji. Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo huko katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahr Bweni, nje kidogo ya Jiji la Zanzibar